6/recent/ticker-posts

BENKI YA NMB TAWI LA MANONGA YAMKABIDHI CHETI CHAPONGEZI MKURUGENZI WA MANISPAA YA SHINYANGA

Na Amoj Media Blog Shinyanga.

Benki ya NMB Tawi la Manonga imekabidhi cheti cha pongezi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze ikiwa ni shukrani kwa mkurugenzi huyo kuichagua banki ya NMB Tawi la Manonga kuwa mshiriki wake bora wa kifedha ndani ya Manispaa hiyo.

Akikabidhi cheti hicho Meneja Huduma kwa Wateja Bw.Emmanuel Makanga amesema kuwa wao kama benki ya NMB Tawi la Manonga wameamua kukabidhi cheti cha shukrani kwa Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake wakuichagua bank ya NMB kama mdau mkubwa na mshiriki bora wa kifedha katika banki hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze akizungumza kwa niaba ya Menejimenti ya Manispaa ya shinyanga ameishukuru benki ya NMB Tawi la Manonga kwa kutambua ushiriki wao wa kuichagua na kuwakabidhi cheti cha pongezi na kuahidi kuwa wataendelea kushirikiana nao katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo.



Post a Comment

0 Comments