6/recent/ticker-posts

RC MACHA AMPONGEZA MENEJA WA TARURA SHINYANGA KWA KUENDELEA KUBORESHA MIUNDO MBINU YA BARABARA.AHAMASISHA USAFI

chanzo Nashinyanga press club blog.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ameupongeza uongozi wa Tarura mkoa wa Shinyanga  kwa kuendelea kuboresha miundo mbinu ya  barabara na kuwasimamia wakandarasi wanao pewa kandarasi za kutekeleza miundombinu ya barabara mkoani humo.

Amebainisha hayo leo Julai 15,2024 wakati akifungua kikao cha bodi ya barabara kilicho fanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo amesema kuwa miundombinu ya barabara inapaswa kuendelea kutunzwa pamoja na kufanyiwa usafi marakwa mara.
\
Aidha Macha amesisitiza utunzwaji wa miundombinu ya barabara zikiwamo taa za barabarani,kuacha kupitisha mifugo,kufanya biashara kando ya barabara,na kudhibiti magari yenye uzito mkubwa ili kutunza miundombinu hiyo.

Katika hatua nyingine Macha amewapongeza Wakuu wa wilaya kwa kuchukua hatua dhidi ya Wakandarasi ambao ni wazembe wanaotekeleza miradi kinyume na makubaliano ya mikataba,na kuwataka waendelee kukaza uzi ili kusimamia kikamilifu fedha za miradi ambazo zinatolewa na Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

“Nawapongeza TARURA kwa utekelezaji wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoani humo 

Kwa upande wake Meneja Wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA)Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Avith Theodory, ameahidi kuwasiliana bodi inayo wasajili wakandarasi ili waendelee kufanya vizuri katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Aidha, akiwasilisha taarifa ya bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwamba walitengewa kiasi cha fedha Sh.bilioni 18.2 lakini wakapokea Sh.bilioni 5.7, huku katika mwaka wa fedha 2024/2025 wakitengewa Sh.bilioni 16.6.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amesisitizwa suala la uzalendeo kwenye usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo,pamoja na kuwapatia zabuni wakandarasi wenye sifa.

Aidha katika kikao hicho iliwasikishwa pia ujenzi wa miradi ya TACTIC katika Manispaa ya Shinyanga na Kahama

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze aliwasilisha mradi wa TACTIC kwenye kikao hicho cha bodi ya barabara.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akichangia mada kwenye kikao hicho cha bodi ya barabara.
Kikao cha bodi ya barabara kikiendelea.
Kikao cha bodi ya barabara kikiendelea.
Kikao cha bodi ya barabara kikiendelea.
Kikao cha bodi ya barabara kikiendelea.
Kikao cha bodi ya barabara kikiendelea.
Kikao cha bodi ya barabara kikiendelea.
Kikao cha bodi ya barabara kikiendelea.
Kikao cha bodi ya barabara kikiendelea.
Kikao cha bodi ya barabara kikiendelea.
Kikao cha bodi ya barabara kikiendelea.

Post a Comment

0 Comments