6/recent/ticker-posts

ASKOFU SANGU AONGOZA MISA YA UPADRISHO KWA MASHEMASI 11 - JIMBO KATOLIKI SHINYANGA,ASISITIZA WAUMINI KULIOMBEA TAIFA LA TANZANIA


Waamini wa kanisa katoliki,Wakristo na watu wote wenye mapenzi mema wameaswa kumuomba Roho Mtakatifu ili awasaidie katika kutenda kazi ya kuhubiri na kutangaza Injili ya Kristo.Hayo yameelezwa na Askofu wa jimbo Katoliki Shinyanga Askofu Liberatus Sangu,wakati wa mahubiri ya Misa ya utoaji wa Daraja la Upadre,tarehe 18 Julai 2024.


Na Amoj Media Blog Shinyanga.
 Mhashamu Askofu Liberatus Sangu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, akitoa homilia yake, kwa waamini wakati wa Adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu ya utoaji Daraja Takatifu ya Upadre kwa mashemasi 11 wa jimbo katoliki la Shinyanga. Katika mahubiri hayo amewahimiza na kutoa wito kwa Wakristo wote na wenye mapenzi mema kuomba Roho Mtakatifu ili awasaidia kutenda kati ya kuhubiri na kutangaza Injili ya Kristo.
Askofu Sangu katika mahubiri hayo amesema kuwa ukimpokea Roho Matakatifu utampeleka kwa watu wengine kwa upendo, huku upendo huo ukianzia kwa familia, Jumuiya na jamii inayokuzunguka. Vile vile amewataka wakristo kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu.
Hata hivyo Askofu  Sangu amewaasa Mapadre wapya na kuwaomba wafanye utume wao kwa upendo, huku wakimuhubiri Kristo, bila kuchoka na wala kukata tamaa,wakiongozwa na Roho Mtakatifu. 
Kwa upande wake aliye wahikuwa mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stiphen Masele akitoa salamu zake ameeleza kuwa kanisa linamchango mkubwa katika jamii katika kuhamasisha amani na kufanya uponyaji. 


Misa ya utolewaji wa Daraja la Upadre imefanyika katika uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Bikra Maria Mwombezi wa neema zote (Maria Mediatrix) Buhangija mjini Shinyanga, na imehudhuriwa na Mapadre, Mashemasi, Watawa, Mafrateri na waamini kutoka sehemu mbalimbali za ndani na nje ya Jimbo la Shinyanga.

Mapadre hao wapya ni Paschal Masunga wa Parokia ya Gula ambaye ametumwa kwenda kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Lubaga mjini Shinyanga, Paschal Mahalagu wa Parokia ya Mwanangi ambaye ametumwa kwenda kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Luka-Bariadi mkoani Simiyu, Paschal Ntungulu wa Parokia ya Shishiyu ambaye ametumwa kwenda kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Maganzo Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Paschal Salyungu wa Parokia ya Mwamapalala ambaye ametumwa kwenda kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Mwanangi wilayani Busega mkoani Simiyu na Peter Sayi wa Parokia ya Mtakatifu John-Bariadi ambaye ametumwa kwenda kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Mhunze wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Wengine ni Japhet Nyarobi wa Parokia ya Mtakatifu Luka-Bariadi ambaye ametumwa kwenda kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Kitangili mjini Shinyanga, Philemon Nkuba wa Parokia ya Buhangija ambaye ametumwa kwenda kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Mwanhuzi Wilayani Meatu mkoani Simiyu, Musa Majura wa Parokia ya Gula ambaye ametumwa kwenda kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Ndala mjini Shinyanga, James Chingila wa Parokia ya Mipa ambaye ametumwa kwenda kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Kilulu Wilayani Bariadi mkoani Simiyu, James kija wa Parokia ya Chamugasa ambaye ametumwa kwenda kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu John-Bariadi mkoani Simiyu na Osward Nkelege wa Parokia ya Bugisi ambaye ametumwa kwenda kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Salawe iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga (Vijijini)



































































































Post a Comment

0 Comments