Meneja was mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (Nssf) mkoa wa Shinyanga anapenda kuwakaribisha wajasiriamali wote Bodaboda,Mama lishe,Baba Lishe,Bajaji,Wakulima,Wafugaji,wachimbaji na wafanya biashara wote kujiunga
na mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) chini ya mpango wa kitaifa wa sekta isiyo rasmi maarufu kama NSSF HIARI
Uchangiaji huu utampa nafasi mjasiriamali huyu kuweza kunufaika na mafao yote yatolewayo na mfuko huu,Kima cha chini cha kuchangia kwa hiari ni sh. elfu 30 kwa mwezi na mwanachama anaruhusiwa kuchangia zaid kadri anavyoweza vilvile anaruhusiwa kuchangia hata kidogo kidogo ili kuweza kukamilisha mchango wake kwa mwezi husika kupitia control number yake
Sambamba na hilo mfuko pia unatoa Mafao ya Matibabu Bure kwa wanachama watakaojiunga na mfuko na kuchangia kwa hiari,Ikiwa Mwanachama atahitaji fao hili pasipo kuwa na familia kima chake cha chini cha uchangiaji kitakuwa ni elfu 30 tu kwa mwezi
Lakini kama mwanachama atahitaji fao hili pamoja na familia yake kimachake cha chini cha uchangiaji kitakuwa elfu 52200 kwa mwezi ambapo watatibiwa watu sita kwenye matibabu hayo ambao ni mwenza wa mwanachama na watoto wanne
Hivyo mwanachama atapata kuweka akiba yake na atapata matibabu bure na akiwa katik umri wa uzee pia atapata pension ya uzeeni
Katika mpango huu wa uchangiaji wa hiari pia wanachama wanawake watanufaika na fao la uzazi kwa kulipwa fedha taslimu na kupata matibabu ya magonjwa yatokanayo na hali ya ujauzito
NSSF TUNAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE,JIUNGE NASI LEO
0 Comments