6/recent/ticker-posts

RADIO KWIZERA YAMKABIDHI CHETI CHA PONGEZI RC MACHA KWA KUFANIKISHA MJADALA WA FUNGUKA TUONGEE BIASHARA SHINYANGA

Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akitoa pongezi kwa mwakilishi wa Radio kwizera mkoa wa Shinyanga Amos John (Mc Mzungu Mweusi ) kwa niaba ya uongozi wa Radio kwizera baada ya kumkabidhi cheti cha pongezi.

Na Amoj Media Blog

Radio Kwizera Fm Kupitia Mwakilishi wake Amos John (Mc Mzungu Mweusi ) Leo Oktoba 4 ,2024 imemkabidhi cheti cha pongezi kwa Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha kwa kutoa ushirikiano uliofanikisha kufana kwa Mjadala wa Funguka Tuongee Biashara Shinyanga uli fanyika Septemba 27,2024 katika uwanja wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Manispaa ya Shinyanga kupitia kipindi cha mchakato na kuwakutanisha wafanya biashara,Wadau wa biashara na Viongozi kutoka katika mamlaka mbalimbali mkoani humo .

Zoezi hilo limefanyika katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kushirikisha Mwandishi wa habari wa Radio Kwizera Shinyanga Amos John akishirikiana na Afisa biashara wa mkoa wa Shinyanga Rose Tungu wakati wa makabidhiano hayo.

Awali Afisa biashara wa mkoa wa Shinyanga Rose Tungu ametoa taarifa ya zoezi hilo kwa Mhe.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga pamoja na kuelezea mafanikio yaliyo patikana kutokana na mjadala huo ulilofanyika kwalengo la kutoa elimu kwa wafanyabiashara .

Kwa upande wake Mhe.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ameupongeza uongozi wa Radio Kwizera kwa kuandaa mjadala huo uliolenga kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara mkoani humo.

Aidha katika mjadala huo ulio endeshwa na Radio Kwizera kupitia kipindi cha Mchakato uliudhuriwa na Afisa biashara wa mkoa wa Shinyanga ,Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ,Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ,Mamlaka ya mapato tanzania (TRA)Taasisi za fedha,Ofisi ya mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga ,Uongozi wa wafugaji ,Machinga ,Vyama vya Siasa wafanyabiashara na wananchi mbalimbali.
Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha baada ya kupokea cheti cha pongezi kutoka kwa mwakilishi wa Radio kwizera mkoa wa Shinyanga Amos John (Mc Mzungu Mweusi ) 
Afisa biashara wa mkoa wa Shinyanga Rose Tungu akitoa taarifa ya mjadala wa Funguka Tuongee biashara Shinyanga kwa kwa Mhe.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Mwakilishi wa Radio kwizera mkoa wa Shinyanga Amos John (Mc Mzungu Mweusi ) akitoa neno la shukrani kwa ushirikiano walio upata kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga. 
Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha baada ya kupokea cheti cha pongezi kutoka kwa mwakilishi wa Radio kwizera mkoa wa Shinyanga Amos John (Mc Mzungu Mweusi ) 
Zoezi la makabidhiano ya cheti cha pongezi likiendelea.


 

Post a Comment

0 Comments