KAMPENI ya "Tuwaambie kabla hawajaharibiwa" inatarajia
kuzinduriwa rasmi kimkoa Okitoba 18 katika uwanja wa Shule ya Msingi Buduhe
halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na kushirikisha viongozi wa
vyama vya siasa ,viongozi wa dini ,Asasi za kiraia na wanafunzi wa Shule za
Msingi na Sekondari na vyuo mkoani humo.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeti Magomi wakati akielezea maandalizi ya uzinduzi wa kampeni hiyo ambapo amefafanua kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga mhe.Anamringi Macha .
0 Comments