Msajili Wavizazi na Vifo Wilkister Mwita akipokea zawadi kutoka Shirika la posta.
Na Amoj Media Shinyanga
Uongozi wa Wakala wa usajili ,Ufilisi na Udhamini (Rita) umepongezwa
na kupewa zawadi na Shirika la posta mkoani Shinyanga kwa utendaji kazi bora na
kuwahudumia vizuri wananchi.
Awali kabla ya kukabidhi zawadi hizo Elizabeth Moye kutoka shirika la posta amesema kuwa wao kama viongozi wa Posta wameamua kuipongeza Ofisi ya vizazi na vifo kwa kazi nzuri wanayo ifanya baada ya kukabidhiwa jukumu la kuwahudumia wananchi kwa kutumia mfumo kufanya Usajili wa vifo,vizazi,na taraka na ndoa kupitia Shirika hilo.
Kwa upande wake Msajili Wavizazi na Vifo Wilkister Mwita ameushukuru uongozi wa shirika la posta kwa kuwapa zawadi hizo huku akieleza kuwa zawadi hizo zimetokana na utendaji kazi wa ofisi hiyo baada ya kuwapa majukumu ya kutumia mfumo kusajili Vifo ,Vizazi ,Taraka na Ndoa kupitia Shirika la posta.Msajili Wavizazi na Vifo Wilkister Mwita akiwa na Katibu tawala wawilaya ya Shinyanga wakipokea zawadi kutoka Shirika la posta.Msajili Wavizazi na Vifo Wilkister Mwita akiwa na Katibu tawala wawilaya ya Shinyanga wakipokea zawadi kutoka Shirika la posta.
0 Comments