6/recent/ticker-posts

MONGELLA AHITIMISHA KAMPENI ZA CCM SHINYANGA 'MSIVAE SARE ZA VYAMA'


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara John Mongella, amewaasa wananchi kutovaa sare na nguo zenye rangi ya chama wakati wakwenda kupiga kura za kuwa chagua viongozi wa serikali za mitaa kwenye maeneo yao .

Mongella amesema hayo wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga,mkutano uliofanyika katika kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga mkoani humo.

 Mongella amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuwachagua viongozi wa serikali zamitaa wanao tokana na CCM ili waweze kuendeleza utekelezaji wa ilani ya chama hicho ulio tekelezwa chini ya uongozi wa Dr.Samia Suluhu Hassan.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajia kufanyika kesho Novemba 27 katika maeneo yate nchini kuwachagua Wenyeviti wa Vijiji Mitaa, Vitongoji,pamoja na wajumbe katika maeneo yao. 

Awali mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi akiwaombea kura wagombea amesema kuwa serikali imetoa fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Shinyanga katika sekta ya Afya ,Elimu ,maji na barabara.









































































Post a Comment

0 Comments