6/recent/ticker-posts

DR.SAMIA/JUMBE HOLIDAY BONANZA KUFANYIKA CCM KAMBARAGE SIKU YA KUFUNGA MWAKA 2024 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2025


DR. SAMIA/JUMBE HOLIDAY BONANZA KUFANYIKA CCM KAMBARAGE SIKU YA KUFUNGA MWAKA 2024 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2025


Na Shinyanga Press Club

BONANZA la michezo Dr.Samia/Jumbe Holiday,litatamatika katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga Desemba 31, ambayo ni siku pia ya kufunga mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025, huku washindi wakitoka na zawadi mbalimbali zikiwamo fedha Taslimu.


Hayo yamebainishwa leo Desemba 27.2024 na Mratibu wa mashindano ya Bonanza hilo Jackline Isaro, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema katika bonanza hilo tayari baadhi ya michezo ilishaanza kufanyika, kuanzia tarehe 24 ambapo tamati ya michezo yote ni Desemba 31 katika uwanja wa CCM Kambarage na washindi wote watapewa zawadi zao.

“Rais Dr,Samia Suluhu Hassan, anahimiza michezo,hivyo kupitia mashindano haya tutaona vipaji mbalimbali,nitoe tu raia kwa wananchi wa shinyanga, wajitokeze kwa wingi kushuhudia michezo hii, ambayo itafanyika bure hakuna kiingilio,”amesema Jackline.

Aidha, ametaja michezo ambayo itachezwa kwenye bonanza hilo kuwa ni mbio za baiskeli, mchezo wa bao,drafti,karata,ususi,Ps Game,Mpira wa pete,kikapu,kufukuza kuku kwa jinsia zote,kushindana kula,Polltable,kucheza mziki.


Ametaja mashindano mengine ya mpira wa miguu kuwa itakuwa kati ya bodaboda dhidi bajaji,bingwa wilaya ‘Ranges’ dhidi ya ngokolo, pamoja na DERBY ya upongoji.

Jackiline ametaja zawadi za washindi kwamba katika mbio za baiskeli mshindi ambayo yatakuwa makundi manne zawadi ni sh.milioni 2.1,mchezo wa bao mshindi wa kwanza sh.100,000,drafti mshindi wa kwanza sh.100,000, karat ash.100,000,msusi sh.100,000, Ps game mshindi wa kwanza sh.200,000 wapili sh.100,000, watatu sh.50,000.


Mpira wa pete, washindi wa kwanza watapewa sh.500,000, kleti za soda 7, mchele kilo 50, washindi wa pili sh.300,000, mchele kilo 50 na soda kleti 7.

Mpira wa kikapu kwa njinsia zote, mshindi wa kwanza atapa sh.500,000 na wapili sh.300,000.


Mchezo wa kufukuza kuku kwa jinsia zote washindi wa kwanza watapa kuku na sh.20,000, na mchezo wa kushinda kula washinda wakwanza watapata sh.20,000, huku mchezo wa polltable mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha sh.100,000, wapili sh.50,000.

Kwa upande wa mpira wa miguu timu ya bodaboda dhidi ya bajaji, mshindi wa kwanza atapata sh.500,000, Ng’ombe mmoja,kleti 7 za soda na mchele kilo 100, wapili sh.300,000, ng’ombe mmoja na mchele kilo 100.


Zawadi zingine bingwa wa wilaya Rangers dhidi ya Ngokolo, mshindi wa kwanza atapata 500,000,Ng’ombe mmoja, mchele kilo 100 na kleti 10 za soda, wapili atapata sh.300,000,Ng’ombe mmoja na soda kleti 10.

DERBY ya upongoji kwamba mshindi wa kwanza atapata sh.1,000,000, Ng’ombe mmoja,mchele kilo 100 na kleti 10 za soda, huku mshindi wa pili akipata sh.500,000,Ng’ombe mmoja, mchele kilo 100 na soda kleti 10.


Nao baadhi ya wanamichezo hao akiwamo James Charles mchezaji wa mpira wa kikapu, amesema bonanza hilo litaibua pamoja na kutambulisha vipaji vingi vya vijana.

TAZAMA PICHA👇👇


Mratibu wa Bonanza la michezo DR.Samia/Jumbe Holiday Jackline Isaro akizungumza na waandishi wa habari.


Mwenyekiti msaidizi wa chama cha waendesha baiskeli Mkoa wa Shinyanga Ngassa Swaganya akizungumzia umuhimu wa bonanza hilo.

Mratibu wa Bonanza la michezo DR.Samia/Jumbe Holiday Jackline Isaro akigawa jezi kwa baadhi ya washiriki wa bonanza hilo.









Post a Comment

0 Comments