6/recent/ticker-posts


Mbunge wa Jimbo la Ngara *Mhe.Ndaisaba G Ruhoro* akiwa ameambatana na viongozi wa CCM Wilaya Chini ya Ndg Vitaris Ndailagije M/kiti wa CCM Ngara  na wataalam kutoka Halmashauri alifanya mkutano wa hadhara Kijiji Cha Nterungwe  kata ya Nyamiaga ambapo alipokea na kutatua kero za wananchi.

 Katika mkutano huo Mh.Ruhoro  akiwa na  wataalam kutoka  RUWASA alikagua mradi wa maji wa Kumuyange kata ya Nyamiaga na Kigina kata ya Ntobeye wenye thamani ya Bilioni 1.6 na ujenzi wa mradi huo kwa eneo la Kumuyange unaendelea vizuri na  umefikia 70% .

Halikadharika Mh.Ruhoro alikagua Shule ya Msingi Shikizi Songambele na kuchangia kiasi Cha fedha  1,500,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wasichana .

Mh.Ruhoro aliwashukuru wananchi wa kata ya Nyamiaga kwa kumchagua *MH.JAMES MAJITA* diwani wa kata hiyo kwani ni miongoni mwa Madiwani wazuri kiutendaji na wanaohakikisha kero za wananchi zinamfikia Mhe.Ruhoro kwa haraka na kushirikiana kuzitatua na kuwaomba wananchi waendelee kumuunga mkono diwani wao .

Pamoja na mambo yote Mh.Ruhoro wakishirikiana na Viongozi wa CCM Kata na Wilaya waliwapokea wanachama wapya kutoka CHADEMA .

Mh.Ruhoro aliendelea kuwasisitiza wananchi kuendelea kuwa na Umoja na mshikamano bila kumsahua *Mama Dr Samia Suluhu Hassan* kwa upendo mkubwa aliouonesha kwa wakazi wa kata ya Nyamiaga kwa kuleta miradi mingi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka minne iliyopita.

Post a Comment

0 Comments