Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro (kushoto) akikabidhi miche ya miti ya matunda kwa maafisa wa kilimo na elimu wa wilaya, pamoja na wataalamu wa kata za Pandagichiza, Iselamagazi na Itwangi.
, Meneja wa Mradi wa Grow-ENRICH, Shukrani Dickson (kulia) akikabidhi miche ya miti ya matunda kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro.Meneja wa Mradi wa Grow-ENRICH, Shukrani Dickson (kulia) akikabidhi miche ya miti ya matunda kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro (mwenye tisheti nyekundu kushoto) , maafisa kutoka World Vision Tanzania, maafisa wa kilimo na elimu wa wilaya, pamoja na wataalamu wa kata za Pandagichiza, Iselamagazi na Itwangi wakiwa wameshikilia pakti za mbegu za mbogamboga
Na Mwandishi Wetu - Shinyanga
Shirika la World Vision Tanzania, kupitia mradi wake wa Grow-ENRICH, limekabidhi miche ya miti ya matunda na mbegu za mbogamboga kwa shule za msingi katika kata za Pandagichiza, Iselamagazi, na Itwangi, wilayani Shinyanga, kwa lengo la kuboresha lishe ya watoto na kuchangia juhudi za utunzaji wa mazingira.
Hafla ya makabidhiano imefanyika leo, Januari 16, 2025, ambapo Shukrani Dickson, Meneja wa Mradi wa Grow-ENRICH, amekabidhi miche ya mipera 520, mipapai 470, na pakiti 195 za mbegu za mbogamboga kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro.
Wakili Mtatiro pia amekabidhi miche hiyo kwa maafisa wa kilimo na elimu wa wilaya, pamoja na wataalamu wa kata za Pandagichiza, Iselamagazi na Itwangi.
Shukrani ameeleza kuwa miche ya matunda ya mipera na mipapai inagawiwa kwa shule zilizoshiriki katika mradi wa awali na kuonyesha uhitaji mkubwa wa kuongezewa miche.
Aidha, mbegu za mbogamboga kama sukumawiki, spinach, na Chinese cabbage zitatumika kuboresha lishe ya watoto na jamii kwa ujumla.
"World Vision Tanzania tunahamasisha kilimo cha mboga za majani na matunda ili kuboresha afya za watoto shuleni na kupunguza utapiamlo," amesema Shukrani.
“Mradi wa Grow-ENRICH unaotekelezwa katika halmashauri za Shinyanga na Kishapu umeweza kununua jumla ya miche 1,215 ya matunda, ikiwa ni mipera 665 na mipapai 550, kwa shule za msingi. Hii ni hatua ya pili ya ugawaji wa miche baada ya miche ya awali kugawiwa kwa shule za kata sita, pamoja na mbegu 2,350 za mbogamboga,” amesema Shukrani.
Amefafanua kuwa shule zilizoshiriki katika mradi na kuonyesha uhitaji wa miche zaidi, hasa zile zenye vyanzo vya maji vya kudumu, zitapata miche hii ili kuendeleza shughuli za kilimo cha matunda na mbogamboga, kwa lengo la kuboresha lishe ya watoto.
“Mradi wa Grow-ENRICH unalenga kuboresha afya na lishe ya watoto, akina mama wanaonyonyesha, na jamii kwa ujumla. Shukrani amesema kuwa kupitia miche ya matunda na mbegu za mbogamboga, World Vision Tanzania inaunga mkono juhudi za serikali katika kutokomeza utapiamlo na kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha lishe kwa watoto na familia zao”,ameongeza Shukrani.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, amelishukuru shirika la World Vision Tanzania kwa msaada wake mkubwa katika kuboresha lishe na afya ya watoto akisema hatua hii inatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na sera za serikali kuhusu lishe.
“Mbegu hizi za mbogamboga na miche ya matunda zitasaidia sana jamii yetu. Tunashukuru kwa msaada huu ambao unalingana na agenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kupambana na utapiamlo na kuboresha afya ya wananchi,” amesema Wakili Mtatiro.
Aidha, amehimiza wananchi na wadau wa kilimo kutumia kwa wingi mboga za majani na matunda katika kila mlo ili kuboresha afya zao na za watoto wao.
“Watumishi, hakikisheni mnasimamia kwa karibu miche hii ili iweze kutoa matunda na kuboresha lishe katika jamii. Nitahitaji ripoti ya maendeleo ya miti na bustani za mbogamboga ndani ya siku 90,” ameongeza Wakili Mtatiro.
Pia, Wakili Mtatiro amewaasa wafanyakazi wa serikali na wa shirika la World Vision Tanzania kuzingatia ulaji bora na kupima afya zao kwa manufaa yao wenyewe, akisisitiza kuwa ulaji bora utasaidia kuboresha afya za jamii nzima na kuwezesha taifa kuwa na nguvu kazi yenye afya.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya miche ya miti ya matunda na mbegu za mbogamboga kwa shule za msingi katika kata za Pandagichiza, Iselamagazi, na Itwangi, wilayani Shinyanga iliyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania, kupitia mradi wake wa Grow-ENRICH kwa lengo la kuboresha lishe ya watoto na kuchangia juhudi za utunzaji wa mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya miche ya miti ya matunda na mbegu za mbogamboga kwa shule za msingi katika kata za Pandagichiza, Iselamagazi, na Itwangi, wilayani Shinyanga

0 Comments