Mhe.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, akifungua rasmi zoezi la Huduma Tembezi ya SAMIA TEACHERS MOBILE CLINIC Shinyanga.
Na Amos John – Amo Blog
Mhe.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, amefungua rasmi zoezi la Huduma Tembezi ya SAMIA TEACHERS MOBILE CLINIC huduma inayo lenga kushughulikia utatuzi wa changamoto wanazo kumbana nazo walimu kwenye maeneo yao.Akifungua rasmi zoezi hilo lililofanyika leo Febuari 16 ,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Walimu Shinyanga (SHYCOM) mkoani humo na kushirikisha walimu zaidi ya 1200 kutoka katika halmashauri 6 za mkoa huoo na mikoa jirani waliofika kwa ajili ya kupata huduma hiyo.
Mhe.Macha amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na CWT kwa kuanzisha utaratibu wa wakuwafata walimu wenye changamoto katika maeneo yao na kuzitatua kwani hali hiyo itachangia kutatua changamoto zinazo wakabili walimu nchini.
Aidha Mhe.Macha ameeleza kuwa kuwa matarajio yake nikuona changamoto nyingi ambazo zilikuwa zikikabili walimu zitapatiwa ufumbuzi kupitia huduma hii, huku akiwaomba walimu kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufaulu wawanafunzi katika mkoa huo.
"Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha maono ya kipevu kwa kuanzisha Huduma Tembezi ya Samia Teachers Mobile Clinic maana huduma hii itasaidia walimu kanapata huduma muhimu kwa wakati na kwa urahisi," alisema Mhe. Macha.
Awali, akitoa salamu za Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Makamu wa Rais, Suleiman Ikomba, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua na kuithamini kazi ya CWT katika utekelezaji wa zoezi hili la kitaifa.
Ikomba amesema kuwa zoezi hili ni muhimu kwa kuhakikisha kwamba changamoto zinazowakumba walimu zinatatuliwa kwa wakati, ili walimu waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na katika mazingira bora.
Ikomba amefafanua kuwa Chama Chawalimu Tanzania CWT kwa kushirikiana na Serikali kwa kutambua mchango wa TASINIA YA Walimu wana jukumu kubwa katika jamii kwa kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu bora, malezi, na ujuzi muhimu kwa maisha yao ya baadaye kwa kuwa kazi yao ni nguzo muhimu katika kujenga kizazi kilichoelimika na jamii yenye maendeleo.
Aidha Ikomba amebainisha kuwa , walimu wanakutana na changamoto nyingi zinazohusiana na mazingira ya kazi, maisha ya kijamii, na hali yao binafsi ,changamoto ambazo zinaweza kuathiri ufanisi wao kazini na kuwazuia kufikia malengo yao ya kuwasaidia wanafunzi .
Kwakulitambua hilo Chama Cha Walimu (CWT) Kimeanzisha Programu Maalumu ya Samia Teacher's Mobile Clinic ambayo kazi yake ni kutatua changamoto za kiutumishi za walimu, Lengo kuu ikiwa ni kuwafikia walimu katika maeneo mbalimbali nchini ili kusikiliza na kutatua changamoto zao .
"Rais ameonesha dhamira ya dhati ya kutatua changamoto za walimu. Tunaamini kwamba zoezi hili litakuwa na manufaa makubwa kwa walimu wote," amesema Komba.
Kwa upande wao Baadhi ya walimu walioshiriki katika huduma ya Kliniki Tembezi ya Msaada wa Samia (Samia Teachers Mobile Clinic) wameelezea furaha yao kwa kupata huduma hii karibu na maeneo yao maana awali walilazimika kutumia gharama kubwa na muda mwingi kusafiri hadi mkoani Dodoma kupata ufumbuzi wa changamoto zao.
Huduma ya Kliniki Tembezi ya Mhe.Dr.Samia inaratibiwa CWT kwa ushirikiana na Ofisi ya Rais, Utumishi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Wizara ya Elimu pamoja na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)na wizara ya fedha ikilenga kuwafikia walimu wote nchini na mkoa wa Shinyanga ukiwa ni mkoa wa 16 kufikiwa na huduma hiyo yenye lengo la kutatua changamoto zao kwa wakati.Makamu wa Rais, wa Chama Cha walimu Tanzania (CWT) Suleiman Ikomba akiendelea kusikiliza changamoto za walimu mkoa wa Shinyanga.
Kaimu katibu mkuu wa Chama Cha walimu Tanzania (CWT)Joseph Misalaba akiwasalimia walimu waliofika kupata huduma ya Samia Teachers Mobile Clinic Shinyanga.
Kaimu Mwekahazina Chama Cha walimu Tanzania (CWT) Nashino Kidudu akiwasalimia walimu waliofika kupata huduma ya Samia Teachers Mobile Clinic Shinyanga.
Mratibu wa Samia Teachers Mobile Clinic Alfred Alexander akiwa wakaribisha walimu na kutoa utaratibu kabla ya kuanza kwa cliniki ya kusikiliza na kutatua changamoto za walimu.
Huduma ya Samia Teachers Mobile Clinic iliendelea kutolewa kwa walimu wa mkoa wa Shinyanga .


0 Comments