6/recent/ticker-posts

HUDUMA YA SAMIA TEACHER'S MOBILE CLINIC YAREJESHA TABASAMU KWA WALIMU WALIOKUWA NA CHANGAMOTO NCHINI

Mamia ya walimu nchini wameitaja huduma ya Samia Teacher’s Mobile Clinic kuwa mkombozi wao, kwani imekuwa na mchango mkubwa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu.
Akizungumza kuhusu lengo la kuanzishwa kwa huduma hii, Makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mwl.Suleiman Ikomba ameeleza kuwa CWT inatambua mchango mkubwa wa walimu katika jamii kwani walimu ni nguzo muhimu katika kuhakikisha watoto wanapata elimu bora, malezi, na ujuzi wa kujiendeleza.
Hata hivyo, walimu wanakutana na changamoto nyingi zinazoweza kuathiri ufanisi wao kazini, ikiwa ni pamoja na changamoto za mazingira ya kazi na hali ya kijamii.

Huduma ya Kliniki Tembezi ya Mhe.Dr.Samia inaratibiwa na  CWT kwa ushirikiana na Ofisi ya Rais, Utumishi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Wizara ya Elimu pamoja na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)na wizara ya fedha ikilenga kuwafikia walimu wote nchini na mkoa wa Simiyu ukiwa ni mkoa wa 17 kufikiwa na huduma hiyo yenye lengo la kutatua changamoto zao kwa wakati.Kaimu katibu mkuu wa Chama Cha walimu Tanzania (CWT)Joseph Misalaba akiwasalimia walimu waliofika kupata huduma ya Samia Teachers Mobile Clinic Shinyanga.

Huduma ya Samia Teacher’s Mobile Clinic imetekelezwa katika mikoa mingi, ambapo walimu wengi wamejitokeza kwa wingi ili kuwasilisha changamoto zao ambapo kwa asilimia kubwa walimu wengi changamoto zao zimepatiwa ufumbuzi.Mratibu wa Samia Teachers Mobile Clinic Alfred Alexander akiwa wakaribisha walimu na kutoa utaratibu kabla ya kuanza kwa cliniki ya kusikiliza na kutatua changamoto za walimu.

Kazi ya Samia Teacher’s Mobile Clinic imepangwa kutekelezwa kwa awamu tano, ambapo hadi sasa awamu nne na yatano inaendelea kutekelezwa katika mikoa ya Dodoma, Tabora, Shinyanga, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, na Morogoro.

Samia Teacher’s Mobile Clinic inaendelea kuwa msaada mkubwa kwa walimu, ikiwasaidia kutatua changamoto za kiutumishi na kuboresha mazingira ya kazi yao kwani huduma hii ni sehemu muhimu ya juhudi za CWT kuhakikisha kuwa walimu wanapata msaada unaohitajika ili kufanikisha malengo yao ya kielimu na kijamii.


 


 

Post a Comment

0 Comments