
Saimon Mashingia ambaye ni mwanasheria kutoka TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, akitoa elimu ya rushwa kuelekea uchaguzi kwa Viongozi wa Jumuiya ya wazazi na wanachama wa chama cha mapinduzi katika kongamano lililo andaliwa na Jumuiya ya wazazi CCM kwa lengo kumpongeza Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake.
Na Amoj Media Shinyanga
Mwanasheria kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga,Saimon Mashingia ametoa elimu ya rushwa kuelekea uchaguzi kwa Viongozi wa Jumuiya ya wazazi na wanachama wa chama cha mapinduzi katika kongamano lililo andaliwa na Jumuiya ya wazazi CCM kwa lengo kumpongeza Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake uliotukuka wenye tija na mafanikio makubwa nchini kiuchumi, kisiasa na kijamii ikiwa nisehemu ya utoaji wa elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa kuelekea Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025.
Elimu hiyo imetolewa leo Jumanne Febuari 25,2025 na Mwanasheria wa TAKUKURU Saimon Mshingia katika ukumbi wa LYAKALE Manispaa ya Shinyanga ikilenga kujadili uzoefu, mchango wa vyombo vya habari katika kuzuia na kupambana na rushwa pamoja na kuweka mikakati ya pamoja kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025.
Saimon Mashingia amesema TAKUKURU inaendelea kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo kuhusu rushwa na madhara yake kwa sababu Tanzania inahitaji kuwa na wananchi wazalendo wasiojihusisha na vitendo vya rushwa.
"Nafasi ya viongozi wa chama na wanachama katika kuzuia Rushwa kwenye uchaguzi ni kuhakikisha mnawaelimisha wanachama wengine kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo rushwa, kushirikiana na TAKUKURU kwenye vita dhidi ya rushwa na kuelimisha jamii kuhusu madhara ya rushwa kwenye uchaguzi",ameongeza Saimon.
Saimon amepamoja na mambo mengine amesema kuwa TAKUKURU Ipo kazini , na iko macho ili kuhakikisha yeyote atakaye jihusisha na vitendo vya rushwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kufikishwa mahakamani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025.

Saimon Mashingia ambaye ni mwanasheria kutoka TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, akitoa elimu ya rushwa kuelekea uchaguzi kwa Viongozi wajumuiya ya wazazi na wanachama wa chama cha mapinduzi.

Viongozi wa CCM wakimsikiliza mwezeshaji kutoka TAKUKURU wakati akitoa elimu ya kuzuia vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu.

Wanachama na viongozi wa CCM wakimsikiliza mwezeshaji kutoka TAKUKURU wakati akitoa elimu ya kuzuia vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu.

Wanachama na viongozi wa CCM wakimsikiliza mwezeshaji kutoka TAKUKURU wakati akitoa elimu ya kuzuia vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu.

Wanachama na viongozi wa CCM wakimsikiliza mwezeshaji kutoka TAKUKURU wakati akitoa elimu ya kuzuia vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu.
0 Comments