6/recent/ticker-posts

BENKI YA NMB TANZANIA YAENDELEA KUWASOGEZEA HUDUMA WANANCHI ,DKT MPANGO AZINDUA TAWI CHANIKA

Benki ya NMB Tanzania inaendelea kuwa karibu yako zaidi! Kwa lengo la kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata huduma bora za kibenki, tumefurahi kuzindua rasmi tawi la NMB Chanika. 

Tawi litakalo hudumia wakazi wa Chanika pamoja na maeneo ya jirani, likiwa ni hatua muhimu katika kuwafikia watu wengi zaidi na kuwapa huduma za kifedha zinazohitajika kwa haraka.

Kuanzishwa kwa tawi la NMB Chanika ,kutarahisisha wateja wa NMB kupata huduma za kibenki kwa urahisi, haraka, na kwa ufanisi. 

Aidha Benki ya NMB imejizatiti kuhakikisha inaendelea kuwa karibu na wananchi nakutoa huduma popote na kwa wakati wowote, hali inayo saidia kuchochea maendeleo ya wananchi,jamii na Taifa kwa ujumla.




Post a Comment

0 Comments