Maadhimisho hayo yamefanyika katika Kanisa la
Mennonite Ngokolo na kuhudhuriwa na waumini kutoka katka makanisa mbalimbali ya
CCT katika Manispaa hiyo.
Katika
maadhimisho hayo, Askofu Bugota amesisitiza umuhimu wa wakristo kudumisha umoja
wa CCT na kupongeza jitihada za wanajumuiya wa makanisa ya Kikristo katika
kutoa huduma za kitume na kijamii kwa jamii.
Bugota amewataka wana CCT kuwa na roho ya
mshikamano, upendo, na kutoa msaada kwa wengine kwa kusaidia jamii,kwa kutoa
huduma za kijamii na za kiroho, ili kuhakikisha ustawi wa jamii nzima.
Askofu Bugota
ametoa wito kwa waumini kuendelea kuliombea taifa la Tanzania katika kipindi
hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kwani ni muhimu kwa waumini wote kuwa na sala
za dhati kwa ajili ya amani ya taifa letu, na kwamba watanzania wanapaswa
kushirikiana na kudumisha umoja kwa manufaa ya Taifa.
Neno la Mungu
lililoongoza maadhimisho hayo limetoka kitabu cha Zaburi 139:14, ambalo
linasema: "Nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu." Neno hili linalenga
kuwakumbusha waumini kuwa kila mtu ameumbwa kwa mpango wa kipekee na wa ajabu
kutoka kwa Mungu, na hivyo kila mmoja anapaswa kuthaminiwa na kuthamini utu
wake.
Maadhimisho
haya yalileta faraja na msukumo kwa waumini wengi, na kwa pamoja walijitolea
kuombea taifa letu, familia zao, na makanisa yao ili iwe na maendeleo endelevu
na Amani.
0 Comments