Pongezi hizo zimetolewa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Bw.Yusuph Juma Mwenda, ambaye ameonyesha kuridhishwa na juhudi za Rais Samia katika kukuza utamaduni wa ulipaji kodi.
Kamishna Mwenda mbali na kumpongeza Dkt.Samia pia amesisitiza umuhimu wa kila raia na mfanyabiashara kutimiza wajibu wake wa kulipa kodi kwa hiari, huku akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa na ustawi wa wananchi.
Aidha, Kamishna
Mkuu amekemea vikali vitendo vya ukwepaji kodi na kusema kuwa Mamlaka ya Mapato
Tanzania itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya watu wote wanaoshiriki vitendo
vya kukwepa kulipa kodi, ili kulinda maslahi ya nchi na kuhakikisha maendeleo
endelevu.
TRA inaendelea
kufanya juhudi za kuhamasisha wananchi na wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa
ulipaji kodi ili kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinatumika vizuri kwa
ajili ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
0 Comments