Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi amesema kodi inayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatumika kujenga miradi ya maendeleo na kuimarisha uchumi wa nchi, hivyo kukwepakodi ni kuikosesha serikali fedha za kutekeleza miradi hiyo.
Mhe. Masindi ameyasema hayo tarehe alipokutana
na maofisa wa TRA wakiongozwa na Kaimu Meneja wa TRA mkoa wa Shinyanga Bw. Ramadhan Sengo kwa lengo la kumpatia mrejesho wa zoezi la elimu ya
kodi ya Mlango kwa Mlango iliyoendeshwa katika wilaya Kishapu.
Mhe. Masindi ametoa wito kwa wafanyabiashara
kutoa ushirikiano kwa TRA wanapopita kuwatembelea kwa lengo la
kuwapatia elimu ya kodiili waweze kulipakodi kwa usahihi na kuiwezesha
serikali kutimiza lengo lake la kuleta maendelea nchini.
'Wafanyakazi wa TRA ni ndugu zetu wanapita
kwenye biashara zetu kuwapa elimu ili kulipa kodi kwa usahihi."amesema
Mhe.Masindi.
0 Comments