Meneja wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro amewakumbusha wafanyabiashara mkoani
Shinyanga ambao bado hawajafanya makadilio ya
kodi kufika TRA na kufanya makadilio yakodi yao katika kipindi hiki cha Malipo ya kodi
kwa awamu ya kwanza kabla ya Tarehe 31 mwezi Mach mwaka huu.
Maro Mbali na kuwahimiza wafanyabiashara kufanya makadilio na
kulipa kodi yao ya awamu ya kwanza pia amewahimiza wafanyabiashara kutunza
kumbukumbu za manunuzi na matumizi ya mashine za EFDs (Electronic Fiscal
Devices) ili kuboresha uwazi na ufanisi katika ulipaji wa kodi.
Amesema kuwa matumizi ya EFDs ni muhimu kwa kuhakikisha kila
muamala unarekodiwa na kodi inalipwa ipasavyo.
Aidha Maro amewashukuru Wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga kwa kutoa
ushirikiano kwa Mamlaka hiyo kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari kwani kufanya hivyo ni kuimarisha
uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla.
0 Comments