Leo tarehe 20 Machi 2025, Mhe.Ahmed
Ally Salum, Mbunge wa Jimbo la Solwa, amefanya ziara katika vijiji vya
Mwogozo na Kano vilivyopo katika kata za Mwenge na Salawe halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga mkoani humo na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo
pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Ziara hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Mwogozo, Kata ya Mwenge mbunge amekagua mradi wa ujenzi wa Zahanati na kuahidi kuchangia mifuko 100 ya saruji ili
kusaidia kukamilisha ujenzi wa Zahanati hiyo ili wananchi wa kata hiyo waweze kupata huduma
bora za afya karibu na maeneo yao.
Pia Mhe. Ahmed ametembelea kijiji cha Kano, kilichopo katika kata ya Salawe, nakukagua ujenzi wa Zahanati inayojengwa katika
kijiji hicho nakuhimiza ushirikiano wa karibu baina ya jamii na serikali ili ujenzi
huo uweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni sehemu
ya mkakati wake wa kuboresha huduma za afya katika jimbo la Solwa kwani sekta
ya afya ni mojawapo ya vipaumbele vyake vikuu.
Pia Mhe.Salum amekutana na wafanyabiashara wa kata ya Salawe na kusikiliza changamoto wanazokutana nazo ambapo ameahidi kuzifisha katika mamlaka husika iliziweze kupatiwa ufumbuzi.
Ahmed amesisitiza kuwa maendeleo ya uchumi wa Solwa yanategemea juhudi za wafanyabiashara, ambao ni sehemu muhimu ya ustawi wa jamii na kuwaomba kukopa mikopo yenye riba nafuu ili kukuza biashara zao na kuchangia ukuaji wauchumi wamkoa na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wakata ya Mwenge na Salawe wamempongeza Mhe.Ahmed kwa kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi huku wakiahidi kumpa ushirikiano wakati wakutekeleza majukumu yake .
Ziara hiyo ya Mhe. Ahmed inadhihirisha jinsi anavyofanya kazi
kwa karibu na wananchi wake, kwa kusikiliza kero zinazo wakabili na kuzitaftia
ufumbuzi.Mhe.Ahmed Ally Salum Mbunge wa Jimbo la Solwa akisikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata ya Salawe na kata ya Mwenge.

















0 Comments