6/recent/ticker-posts

SHANGWE ZA TAWALA KHAMIS HAJI AKIRUDISHA FOMU YA KUGOMBEA UDIWANI KATA YA KAMBARAGE KWA KUTUMIA USAFIRI WA PUNDA



Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khamisi Haji, ametimiza masharti ya kikanuni ya chama chake kwa kukamilisha hatua ya awali ya mchakato wa kugombea nafasi ya udiwani katika Kata ya Kambarage, Manispaa ya Shinyanga, baada ya kurejesha rasmi fomu za uteuzi.

Haji amerejesha fomu hiyo Augosti 27 katika ofisi za CCM za kata hiyo,hatua inayotafsiriwa kama mwanzo wa safari yake ya kuwania nafasi ya kuongoza wananchi kupitia chama cha Mapinduzi.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu, Khamisi Haji amesema kuwa ameamua kuomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa Kambarage kupitia nafasi ya udiwani kwa lengo la kushirikiana nao kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, biashara na miundombinu ya barabara.

“Ni dhamira yangu ya dhati kuhakikisha kuwa wananchi wa Kambarage wananufaika zaidi na fursa mbalimbali za maendeleo zinazopatikana kupitia serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwani nimejipanga kusikiliza kero zenu na kuzitafutia majibu kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama na serikali,” amesema Haji.

Aidha, baadhi ya wanachama wa CCM waliomsindikiza Haji wakati wa zoezi hilo wameeleza imani yao kwa kada huyo, kuwa kurejesha kwake fomu ni ishara ya utayari wake kwenda kuwatumikia wananchi wakata ya kambarage.


TAZAMA PICHA ZOTE HAPA WAKATI KHAMISI HAJI AKIRUDISHA FUMU







































Post a Comment

0 Comments