6/recent/ticker-posts

MKURUGENZI KOM SCHOOLS AAHIDI MAKUBWA KWA WASAFIRISHAJI , DTO SHINYANGA AWAPIGA MSASA MADEREVA BAJAJI NA BODABODA


Mgeni rasmi wa tamasha la Simba na Yanga , Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, ASP Zainab Mangala na mkurugenzi wa Kom Schools Jakton Koy wakishuhudia mpambano wa Bajaji na Bodaboda.

Katika shamrashamra za kuelekea Simba Day na Yanga Day, timu ya Bajaji FC imeonyesha ubabe uwanjani baada ya kuichapa Bodaboda FC kwa mabao 3–0 katika tamasha kubwa la michezo lililofanyika kwenye Uwanja wa Sekondari Kom, Manispaa ya Shinyanga.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Mkurugenzi wa Kom Schools, Jakton Koy, kwa lengo la kuwaunganisha wasafirishaji wa bodaboda na bajaji,huku likihamasisha mshikamano na burudani kupitia mchezo wa mpira wa miguu.

Katika mchezo huo uliovutia mashabiki wengi, Bajaji FC imeonyesha umahiri mkubwa na kuondoka na zawadi ya mbuzi mnyama na crate mbili za soda, huku wapinzani wao Bodaboda FC wakijipatia crate tatu za soda kwa ushiriki wao.

Mgeni rasmi wa tamasha hilo, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, ASP Zainab Mangala, amewataka waendesha pikipiki na bajaji kufanya kazi zao kwa kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

Amewasihi kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia, akisisitiza umuhimu wa kuunga mkono kampeni ya “Waambie Kabla Hawajaharibika” inayoendeshwa na Jeshi la Polisi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kom Schools, Jakton Koy ameahidi kuongeza udhamini wa tamasha hilo kwa ukubwa zaidi katika miaka ijayo, huku akiwataka wasafirishaji kuwa mabalozi wa kueneza habari njema kuhusu mchango wa shule hiyo katika sekta ya elimu.

Nao baadhi ya waendesha bodaboda na bajaji wamemshukuru Koy kwa moyo wake wa kudhamini tamasha hilo, na kuwataka wadau wengine kuunga mkono jitihada kama hizo ili kuinua michezo na kudumisha mshikamano katika jamii.

Aidha, wadau wa michezo kutoka ASCO Lounge pamoja na Gvenwear wameshiriki kuunga mkono tamasha hilo kwa kuongeza zawadi kwa washindi wa mpambano huo, hatua iliyoongeza hamasa na mvuto wa mashindano.

Mgeni rasmi wa tamasha la Simba na Yanga , Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, ASP Zainab Mangala na Mkurugenzi wa Kom Schools, Jakton Koy wakiwa kwenye picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo.

Mgeni rasmi wa tamasha la Simba na Yanga , Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, ASP Zainab Mangala akizungumza na madereva Bajaji na Pikipiki katika Tamasha hilo.

Mgeni rasmi wa tamasha la Simba na Yanga , Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, ASP Zainab Mangala na mkurugenzi wa Kom Schools Jakton Koy wakishuhudia mpambano wa Bajaji na Bodaboda katika tamasha hilo.

Mkurugenzi wa Kom Schools Jakton Koy akizungumza na madereva Bajaji na Bodaboda.

Mgeni rasmi wa tamasha la Simba na Yanga , Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, ASP Zainab Mangala akiwa na maafande wengine.

Mgeni rasmi wa tamasha la Simba na Yanga , Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, ASP Zainab Mangala akiwa na maafande wengine.



Timu ya Madereva Bajaji wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Timu ya Madereva Pikipiki wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Timu ya Madereva Pikipiki wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Mpambano kati ya madereva Pikipiki na Bajaji ukiendelea.

Mpambano kati ya madereva Pikipiki na Bajaji ukiendelea.

Post a Comment

0 Comments