6/recent/ticker-posts

MISA TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 30 IKIJIVUNIA MAFANIKIO MAKUBWA...SERIKALI YATAKA WAANDISHI WA HABARI WAPEWE SEMINA NYINGI

 



Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari- MAELEZO Gerson Msigwa.

Na Kadama Malunde - Dodoma

Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), imeadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 huku ikijivunia makubwa iliyoyafikia kwa kipindi hicho.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Alhamisi Mei 25,2023 katika ukumbi wa New Dodoma Hotel Jijini Dodoma yakihudhuriwa na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari, pamoja na wanachama wa Misa Tanzania ambapo mgeni rasmi alikuwa Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari- MAELEZO Gerson Msigwa kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekonolojia ya Habari, Nape Nnauye.


Akizungumza wakati akifungua Maadhimisho ya Miaka 30 ya MISA Tanzania, Msigwa amesema Serikali kupitia Wizara ya habari Teknolojia na Mawasiliano itaendelea kushirikiana vyema na waandishi wa habari katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili pamoja na kutekeleza Maagizo ya Rais Samia ya kuifanyia Marekebisho ya Sheria ya huduma za habari ya mwaka (2016) kwa kurekebisha vifungu ambavyo vinabinya uhuru wa habari na kujieleza.

Amesema serikali inaendelea kuboresha mazingira ya vyombo vya habari huku akisisitiza kuwa tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani hakuna chombo kilichofungiwa na vilivyokuwa vimefungiwa vimefunguliwa.


“Serikali chini ya Rais Samia inatambua kazi nzuri inayofanywa na waandishi wa habari na ipo bega kwa bega na Waandishi wa habari na ndiyo maana ndani ya miaka miwili ya utawala wake hamjasikia chombo chochote cha habari ambacho kimefungiwa na Magazeti ambayo yalifungiwa yamefunguliwa”, amesema Msigwa.

Post a Comment

0 Comments