6/recent/ticker-posts

UWANJA WA NDEGE IBADAKULI - SHINYANGA WAANZA KUJENGWA ,WADAU WA USAFIRI WA ANGA WAPONGEZA.


Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa. Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli. 

Namalunde blog.

Ukarabati na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga umeanza ukitarajiwa kurahisisha usafiri kwa wananchi pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi hususani katika sekta ya madini mkoani na taifa kwa ujumla.


Akizungumza leo Mei 30,2023, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kwenye Mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS uliofanyika katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga amesema ni muhimu ujenzi wa uwanja wa Ndege Shinyanga uzingatie viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya pesa na ukamilike ndani ya wakati.


“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege. Kwa muda mrefu watu wa Shinyanga wamekuwa na shauku kubwa ya kupata uwanja wa ndege kwani wamekuwa wakilazimika kusafiri kwenda mkoani Mwanza kupanda ndege umbali wa kilomita 164”,amesema Samizi.




Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati Wadau wa Usafiri wa Anga wakitembelea uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

“Tumekutana hapa kwa ajili ya mkutano wa wadau wa usafiri wa anga lakini pia mkutano huu tuutumie kama uzinduzi rasmi wa ujenzi wa mradi huu. Rai yangu kwa wananchi wa Shinyanga ni kuchangamkia fursa kupitia mradi huu, tengenezeni shughuli ambazo zitachochea uchumi na tuhakikishe tunaulinda mradi huu”,ameongeza Samizi.







 

Post a Comment

0 Comments