6/recent/ticker-posts

WANANCHI MULEBA WAPEWA MBINU ZA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO.  

      Namwandishi wetu Muleba.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Deo Kisaka akikabidhi vifaa vya kujikinga na magonjwa ya mripuko katika Zahati ya Kerebe.

 Ofisi ya  Mganga mkuu halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera imefanya ziara katika Visiwa vya Goziba, Kerebe na Nyaburo  vilivyo ndani ya Ziwa Victoria  kwa ajili ya kujionea namna  elimu ya afya ilivyozaa matunda katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika visiwa hivyo ikiwemo ugonjwa wa Marburg  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja Unicef na Mv Jubilee hope medical ship program  chini ya kanisa la AIC Tanzania.

 Akiongoza timu hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Deo Kisaka amesema  ni muhimu kuweka mazingira katika hali ya usafi katika kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama vile kuhara,kipindupindu, kuumwa tumbo.

 Kwa upande wao baadhi ya viongozi katika visiwa hivyo akiwemo Afisa mtendaji Kata ya Kerebe  Kanali Sefu , Diwani Kata ya Kerebe Sudy Said  pamoja na Diwani Kata ya Goziba  Mataba Mataba wamezungumzia  namna serikali ilivyochukua  hatua katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko .

Nao  baadhi ya wananchi wanao ishi karibu na visiwa hivyo wameishukuru Serikali kwa kuondoa hofu na taharuki na kujikita zaidi katika utoaji wa elimu ya afya hali ambayo imesabibisha kuongeza uzingatiaji wa  kanuni za afya na kuendelea na shughuli za kila siku.

 Katika kampeni hiyo jumla ya wakazi 89 wa kisiwa cha Goziba ,wakazi 161 wa kisiwa cha kerebe na wanafunzi 124 kutoka shule ya msingi Goziba wamefikiwa nakupatiwa elimu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko katika kisiwa hicho.



 

Picha ya pamoja ya watalaam wa Afya kutoka Wilaya ya Muleba wakipiga picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kata ya Kerebe kwenye ofisi ya Kijiji Cha Kerebe.

Post a Comment

0 Comments