6/recent/ticker-posts

BENKI YA NMB TAWI LA MANONGA YAIBUKA NA MWAROBAINI WA KUWAEPUSHA WANAWAKE NA MIKOPO UMIZA SHINYANGA

Afisa Masoko wa Benki ya NMB Tawi la Manonga Albini Mpona ameshiriki kongamano la wanawake Manispaa ya Shinyanga na kutoa elimu kwa wanawake hao juu ya namna wanavyo weza kunufaika na huduma bora zinazo tolewa na Benki ya NMB, hali itakayo wasaidia wanawake hao kujiepusha na mikopo umiza.

Aidha Mpona ametumia kongamano hilo kutaja miongoni mwa akaunti ambazo zinaweza kuwa faa wanawake , kuwa ni pamoja na Akaunti ya NMB Pesa Akaunti ,Akaunti ya Kikundi , Mtoto Akaunti na Akaunti nyingine za NMB ambazo zinamuwezesha mnufaaika wa Benki ya NMB kupata manufaa ya fuatayo.

✅Mikopo isiyo na dhamana

✅Kutoa, kuweka au kutuma pesa

✅Kulipia bili 

Afisa Masoko wa Benki ya NMB Tawi la Manonga Albini Mpona akitoa elimu kwa wanawake walio fika katika kongamano hilo. 

Post a Comment

0 Comments