6/recent/ticker-posts

MENEJA AGRICOM ATANGAZA FURSA KWA WAKULIMA KATIKA MAADHIMISHO YA JUKWAA LA MAENDELEO YA USHIRIKA MKOA WA SHINYANGA

Meneja wa Kampuni ya Agricom inayo jihusisha na uuzaji wa Zana bora za kilimo Kanda ya Ziwa Christina Mabula akitoa salamu za kampuni kwenye maadhimisho ya jukwaa la maendeleo ya ushirika mkoa wa Shinyanga 

Na Amo Blog Shinyanga.

Meneja wa Kampuni ya Agricom inayo jihusisha na uuzaji wa Zana za kilimo Kanda ya Ziwa Christina Mabula ametumia jukwaa la maendeleo ya ushirika kuwaomba wanaushirika kutumia fursa zinazo patikana katika kampuni hiyo kulima kilimo chenye tija hali itakayo wawezesha kupata mavuno mengi zaidi na kujikwamua kiuchumi.

Mabula amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Jukwaa la maendeleo ya Ushirika lililofanyika Marchi 21,2024 katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi Shinyanga, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Juma Mokili Juma akimwakilisha Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk. Benson Ndiyege.katika maadhimisho hayo.

Aidha Mabula ameongeza kuwa kampuni ya Agricom inazo fursa nyingi ambazo zinawa faa wakulima ikiwemo zana za kilimo na kuwaomba wakulima kuendelea kuiamini kampuni hiyo maana inashirikiana na taasisi za fedha kuwawezesha wakulima zana bora za kilimo kwa gharama nafuu.


Nao baadhi ya wakulima wameipongeza kampuni ya Agricom kwa kuendelea kuwajali wakulima kwa kutoa  zana bora za kilimo haili ambayo imewasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na kilimo cha mazoea.
Wakulima ambao ni wanaushirika wakimsikiliza meneja wa Kampuni ya Agricom wakati wa salamu za kampuni.


Wakulima ambao ni wanaushirika wakimsikiliza meneja wa Kampuni ya Agricom wakati wa salamu za kampuni.

Post a Comment

0 Comments