Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Janeth Magomi akikabidhi matofali na pesa kwa Diwani wa kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mussa Elias kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha polisi katika kata hiyo.
Akikabidhi msaada huo leo Machi 22,2024 kwa uongozi wa kijiji na kata Kamanda Magomi amesema kuwa amekabidhi msaada huo ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi yake aliyoitoa ya kuwaunga mkono wananchi wa kata ya Kolandoto katika ujenzi wa kituo cha polisi.
Aidha kamanda Magomi amewataka viongozi wa kata na vijiji na mitaa katika kata ya Kolandoto kushikamana katika ujenzi wa kituo cha polisi ili kituo hicho kiweze kukamilika kwa wakati hali itakayosaidia kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa wakazi wa kata ya Kolandoto na maeneo jirani.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kolandoto Mussa Elias akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo amempongeza Kamanda Magomi kwa kutoa msaada huo hku akieleza kuwa msaada huo utakuwa chachu kwa wananchi kushikamana ili waweze kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha polisi kwa wakati.
0 Comments