6/recent/ticker-posts

STAMIGOLD BIHARAMULO MINE YASHINDA TUZO ZA USALAMA NA AFYA MAHALI PAKAZI (OSHA)

Afisa Mwandamizi wa Usalama, Afya, Mafunzo na Uokoaji katika Mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo Fred Makwebeta akitoa elimu kwa wananchi walio tembelea banda la STAMIGOLD.
Mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo uliopo mkoani Kagera Umewashangaza watuwengi zaidi katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali paKazi kwa kuweza kufikisha Masaa 12,322,625 pasipo kupoteza muda wa kazi.

Adha Mgodi huo umepata tuzo katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Usalama na Afya Mahali Pakazi (OSHA) ya 2024 iliyo fanyika jijini Ausha ambapo Mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo umeshinda tuzo ya Usalama na Afya Mahali Pakazi Mwaka 2024.

Maonyesho ya OSHA yamefanyika Jijini humo ambapo mgeni Rasmi alikuwa ni Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya waziri mkuu Kazi ,ijana, Ajira na watu wenye ulemavu Patrobas Katambi aliye mwakilisha waziri Deogratius Ndejembi .

Baada ya zoezi la utoaji wa tuzo hizo Wafanya kazi wa Mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo wameonyesha furaha yao baada ya kushinda tuzo hiyo huku wakieleza kuwa itakuwa ni motisha ya kuendelea kufanya viziri kwa kuimarisha Usalama na Afya mahali pakazi kwa wafanyakazi wao amesema Afisa Mwandamizi wa Usalama, Afya, Mafunzo na Uokoaji katika Mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo Fred Makwebeta baada ya kupokea tuzo hiyo.

Post a Comment

0 Comments