6/recent/ticker-posts

MABALOZI WA USALAMA BARABARANI SHINYANGA WATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI ,NA KUTEMBELEA WAFUNGWA NA MAJERUHI HOSPITALI

Ilikupambana na ajali zisizo kuwa za lazima Mabalozi wa Usalama Barabarani mkoani Shinyanga umetoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Ushirika na Shule ya Msingi Town zilizopo halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani humo.

Akieleza lengo la kutoa elimu hiyo mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Selfu Nasoro ameeleza kuwa wameamua kutoa elimu hiyo ikiwa ni sehemu ya kupambana na ajali zinazo tokea kutokana na uzembe wa madereva wa vyombo vya moto. 

Kwa upande wake Mwalimu Meshaki Helmani ambaye ni mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Town pamoja na mwalimu Christina Mbuye mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Ushirika wanaeleza umuhimu wa mafunzo hayo yaliyo tolewa na mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga kuwa yatasaidia kupunguza ajali za barabarani na kuwajengea uelewa wanafunzi juu ya namna ya kutoa taarifa pindi wanapo baini uwepo wamatukio ya ajali katika maeneo ya shule na nje ya shule.

Mbali na Mabalozi wa Usalama barabarani kutoa elimu hiyo pia wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa wanafunzi wa shule hizo pamoja na kutembelea Wafungwa waliopo katika gereza la mhumbu na wagonjwa majeruhi waluio lazwa katika wodi ya majeruhi hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga mwawaza.

TAZAMA PICHA ZAMATUKIO YOTE HAPA CHINI 
























































Post a Comment

0 Comments