6/recent/ticker-posts

CHOMOKA ATUMIA MAHAFALI YA KWANZA KUMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUMTEUA NA KUMLETA KAGUNZE MANISPAA YA SHINYANGA

Mkurugenzi  wa Chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga Zahoro Chomoka akiongoza wakufunzi wachuo hicho kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayo ifanya.

Na Mwandishi wetu Amoj Media Shinyanga.


Mkurugenzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga Zahoro Chomoka amempongeza kwa dhati Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri na njema anayoifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi wote wa Tanzania ikiwemo kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa wazawa nchini.

Chomoka amesema hayo katika Mahafali ya kwanza ya chuo yaliyofanyika Desemba 14, 2024 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga yaliyo hudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi, viongozi wa Dini na wadau wa maendeleo ambapo pamoja na mambo mengine Mkurugenzi  wa Chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga Zahoro Chomoka amempongeza kwa dhati Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua na kumleta mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze kwani uwepo wake umesaidia kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wazawa wanao wekeza katika sekta mbalimbali ndani ya Manispaa hiyo hali ambayo inaendelea kuchochea maendeleo ya wanashinyanga.

Chomoka ameeleza kuwa wakati uongozi wa Chuo hicho ukiendelea na mipango yake ya kuanzisha ujenzi wachuo hicho katika mkoa wa Shinyanga wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa mkurugenzi huyo hali ambayo imewapa nguvu ya kuwekeza katika mkoa wa Shinyanga bila wasiwasi kwa kuwa amewapa eneo maalum kwa ajili ya kujenga chuo hicho ambacho kitasaidia kuongeza mzunguko wa kiuchumi katika Manispaa ya Shinyanga ,mkoa na Taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Ramadhani Masumbuko amesema kuwa wao kama madiwani kwa kushirikiana na Mhe. Patrobass Katambi mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) wataendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wazawa ambao wanakuja kuwekeza katika Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa maeneo ya kuwekeza bado yao  ,nakufanya hivyo nikuongeza mzunguko wa kiuchumi na maendeleo ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa nisehemu ya kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi.


Pia niwaombe wazazi na walezi kuleta watoto wenu katika chuo hiki ambacho kinatoa elimu bora na kuwawezesha vijana kumudu soko la ushindani kwa kujiajiri baada ya kumaliza masomo yao ya Astashahada na Stashahada katika chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga.Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Ramadhani Masumbuko akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza katika chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga.


TAZAMA PICHA ZA MAHAFALI YA KWANZA CHUO CHA MTAKATIFU JOSEPH SHINYANGA.















































Post a Comment

0 Comments