Mkuu wa Chuo Cha Mtakatifu Joseph Shinyanga Miraji Zahoro Chomoka akieleza mafanikio ya chuo hicho katika mahafali ya kwanza ya chuo Cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga .
hitimu wa Astashahada na Stashada katika.
Na Amoj Media Shinyanga.( 0762421248)
Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga yamefanyika huku wanafunzi wafani mbalimbali zaidi ya miambili (200) kutoka mikoa tofauti ya Tanzania wamehitimu elimu yao katika ngazi ya Astashahada na Stashahada katika chuo hicho.
Mahafali hayo ya Kwanza ya Chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga kilichopo Jengo la Chama Cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Shinyanga Gholofa ya tatu na ya nne Shinyanga Mjini yamefanyika leo Jumamosi Desemba 14,2024 katika ukumbi uliopo katika jengo hilo ambapo mgeni rasmi alikuwa Msitahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko .
Awali akitoa taarifa ya chuo hicho mkurugenzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga Miraji Zahoro Chomoka amewaomba wananchi kuchangamkia fursa zinazo patikana katika Chuo hicho ambacho kinatoa elimu na kumuandaa mwanachuo kupambana katika soko la ajira.
“Chuo chetu kinapokea wanafunzi wa fani mbalimbali ikiwemo elimu ya Malezi ya watoto ,Uandishi wa habari na utangazaji ,Manunuzi na Ugavi ,Usimamizi rasilimali watu pamoja na Tehama ambapo mwanafunzi wakujiunga katika fani hizo anatakiwa kuwa na ufaulu wa D 4 na kuendelea.”,amesema Chomoka .
Akiwatunuku vyeti wahitimu wahao ambao wamehitimu elimu ya Astashahada na Stashahada Mgeni rasmi ambaye ni Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko ameupongez uongozi wa Chuo Cha Mtakatifu Joseph kwa kutoa elimu bora kwa vijana wakitanzania nakuahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi wa chuo hicho ikiwa ni sehemu ya kuungamkono juhudi za mbeba maono ambaye ni mkurugenzi wa chuo hicho ili waweze kufikia malengo na matarajio ya chuo.
“Hiini fursa nyingine mmeileta Shinyanga ,itasaidia wanashinyanga ,hivyo niwaombe wanashinyanga mkiamini chuo hiki na kuwaleta watoto wenu walio hitimu elimuya sekondari ili wajiunge na chuo hiki kinacho toa kozimbalimbali .
Pia Masumbuko amewashauri wahitimu kutumia ujuzi walio upata katika kuitumikia jamii na kuchochea maendeleo maana ninaimani mmejifunza mambo mengi na mmepata ujuzi wa kutosha kutoka kwa walimu wenye ujuzi na uzoefu waliopo katika chuo hiki cha Mtakatifu Joseph.
Wahitimu wa Astashahada na Stashada katika chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga wakiwa kwenye maandsamano wakati wa mahafali.
Wakufunzi katika chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga wakiwa kwenye mmahafali.
Wahitimu wa Astashahada na Stashada katika chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga wakiwa kwenye maandsamano wakati wa mahafali.Wahitimu wa Astashahada na Stashada katika chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga wakiwa kwenye maandsamano wakati wa mahafali.
Wahitimu wa Astashahada na Stashada katika chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga wakiwa kwenye maandsamano wakati wa mahafali.
Wakufunzi katika chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga wakiwa kwenye maandsamano wakati wa mahafali.
Picha ya pamoja wakati wa mahafali.
Wahitimu wa Astashahada na Stashada katika chuo cha Mtakatifu Joseph Kampasi ya Shinyanga wakiwa kwenye maandsamano wakati wa mahafali.
0 Comments