6/recent/ticker-posts

JOSEPH ASSEY ACHAGULIWA KWA KISHINDO KUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MPIRA WAMIGUU WILAYA YA SHINYANGA

Joseph Assey aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga akizungumza baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa SHIDIFA.

Na Amo Blog Shinyanga.
 
Wanachama wa chama cha mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga wamemchagua Joseph Assey kuwa mwenyekiti wa Chama cha mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga (SHIDIFA)

Uchaguzi huo umefanyika leo Desemba 24 katika ukumbi wa Utulivu uliopo katika eneo la Nguzo nane Manispaa ya Shinyanga ambapo kwa umoja wao wanachama wamemchagua Joseph Assey kuwa mwenyekiti wa SHIDIFA baada ya Assey kuongoza chama hicho akiwa kaimu mwenyekiti kwa kipindi kadhaa na kuchochea maendeleo ya mpira wamiguu katika wilaya ya Shinyanga.
Akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa Assey amesema kuwa ataendelea atatumia ujuzi wake wakati wa uongozi wake ili kuchochea maendeleo ya mpira wa Shinyanga ikiwa nipamoja na kutafta wadau wamichezo watakao dhamini mashindano mbalimbali ili kuchochea na kuinua vipaji kwa vijana wa Shinyanga.
Aidha Assey amesema kuwa pia atatumia uzoefu wake kuzishawishi timu ambazo bado hazijafanya usajili kufanya usajili ili ziweze kuwa na uhalali wakushiriki katika mashindano mbalimbai.

Kwa upande wake Afisa Michezo wa Manispaa ya Shinyanga, Anord Rukiza akizungumza baada ya uchaguzi kumalizika amemuomba mwenyekiti aliye chaguliwa kudumisha umoja na mshikamano baina ya timu moja na timu nyingine ikiwa ni njia moja wapo itakayo saidia kudumisha mshikamano na kuchochea maendeleo ya mpira wa wilaya ya Shinyanga.

Afisa Michezo wa Manispaa ya Shinyanga, Anord Rukiza akizungumza baada ya uchaguzi kumalizika .

Post a Comment

0 Comments