6/recent/ticker-posts

JACKLINE ISARO ANADI SERA ZA CCM KATA YA NGOKOLO


Mgombea wa Udiwani Kata ya Ngokolo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jackline Isaro, ameendelea kunadi sera na Ilani ya CCM kwa wananchi wa kata hiyo akiwataka kukipa kura chama hicho kwenye uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.

Katika mkutano wake wa kampeni uliohudhuriwa na wanachama na wapenzi wa CCM, Jackline Isaro amewaeleza wananchi kuwa utekelezaji wa Ilani ya CCM ndio msingi wa maendeleo ya kweli, akiahidi kusimamia miradi ya kijamii pamoja na kuibua fursa za kiuchumi kwa vijana na wanawake.

Aidha, Jackline Isaro amewaomba wananchi wa Kata ya Ngokolo kumpa kura za ushindi, huku pia akisisitiza umuhimu wa kuwachagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwaletea maendeleo Watanzania, pamoja na Patrobas Katambi ambaye ni mgombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM.

Amewasihi wananchi kuendeleza mshikamano kwa kuhakikisha CCM inaibuka na ushindi wa kishindo katika ngazi zote za uongozi.







Post a Comment

0 Comments